Ajira Ajira Ajira......walimu 2014/2015....


JAMHURI YAMUUGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA
 https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c2/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg/220px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU AJIRA MPYA ZA
WALIMU WA MASOMO YA HISABATI NA SAYANSI KWA MWAKA
2016/2017
Serikali kupitia
Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa
Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017.
Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi
ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo
tarehe 01 Desemba, 2016.
Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya
Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada.
Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa
Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18
Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na
vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI),
vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya
Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa.
Angalizo :
i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi
waliohitimu hadi mwaka 2014/2015
ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao
makuu ya Halmashauri.
iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae
kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18
Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao
zitajazwa na mwalimu mwingine.
v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.

Majina ya Walimu hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais￾TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
 
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais TAMISEMI

Doppler the blog imekuwekea hapa link zote.................HAPA

Walimu wa Degree download hapa
walimu wa Diploma hapa




Maoni

Ulizikosa hizi ....

On-Line Learning with Mr.Juma A. Mkiwa in BIOLOGY